Hapo kabla tulisoma kwa kirefu kuhusu vidonda vya tumbo, kisha tukasoma kuhusu dawa mbadala ya vidonda vya tumbo, tukasoma tena kuhusu chakula cha mgonjwa wa vidonda vya tumbo, na leo tunaendelea kuangalia dalili za ugonjwa wa vidonda vya tumbo.
Dalili
zitakazokufanya ujihisi una vidonda vya tumbo ni pamoja na;
1.
Kuchoka choka sana bila sababu maalum
2. Kuuma mgongo au kiuno
3. Kupungukiwa au kupoteza kabisa nguvu za kijinsia
4. Kizunguzungu
5. Kukosa usingizi
6. Usingizi wa mara kwa mara
7.
Maumivu makali sehemu ya mwili
8. Kifua kwa ndani kana kwamba unachomwa na kitu cha
moto au chenye ncha kali. Maumivu hayo wakati mwingine hutokeza mgongoni na
huchoma kama sindano yenye sumu na kuacha maumivu makali
9. Kichefuchefu
10.
Kiungulia
11.
Tumbo kujaa gesi
12.
Tumbo kuwaka moto
13.
Maumivu makali sehemu kilipo kidonda
14.
Kukosa choo au kupata choo kwa shida
tena kikiwa kigumu na chenye kukatika kama cha mbuzi
15.
Kutapika nyongo
16.
Kutapika damu au kuharisha
17.
Sehemu za mwili kupata ganzi
18.
Kukosa hamu ya kula
19.
Kula kupita kiasi
20.
Kusahahu sahau na
21.
Hasira bila sababu.
Kwa kweli ni vigumu
kueleza maumivu yote apatayo mgonjwa wa vidonda vya tumbo hasa kwa mwenye
vidonda sugu kwani hakuna hata kiungo kimoja mwilini atakachokuambia ni kizima

0 comments :
Post a Comment